Jumatatu 9 Machi 2026 - 17:15
Ayatullah udhma Jawad A'moli atuma ujumbe wa pongezi kutokana na kuchaguliwa Kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Iran

Hawza/ Mtukufu Ayatullah udhma Jawad A'moli kutokana na kuchaguliwa Sayyid Mujtaba Khamenei kama Kiongozi wa tatu wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, amesema kuwa: Mfumo wa Uimamu na ummah ni zawadi bora katika uhai.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa Ayatullah udhma Jawad A'muli, kutokana na kuchaguliwa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei kama Kiongozi wa tatu wa Mapinduzi ya Kiislamu Irani, ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mola Mtukufu

Mfumo wa Uimamu na ummah ni miongoni mwa zawadi bora zaidi katika maisha, ni matumaini yangu viongozi waliotangulia wafufuliwe na Viongozi wa Kiungu, na kile ambacho Baraza la wataalamu wa Uongozi limekichagua, kiwe ni chenye kusalia na kukusanya mambo yote yajayo.

Na amani iwe juu ya wenye kufuata uongofu


Jawad A'muli'
19 Ramdhan 1447/ 18 Isfand 1404/ 9 March 2026.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha